Wanafunzi 300 wanakaa chini Shule ya Msingi Nyamalunda Sengerema
18 February 2024, 7:13 pm
Licha ya juhudi za Serkali kujenga na kukarabati baadhi ya vyumba vya madarasa Shule za mssingi nchini baadhi ya shule zinachangamoto kubwa ya Madawati halii inayo pellekea wanafunzi wa shulle hizo kukaa chiini.
Na:Emmanuel Twimanye
Wanafunzi mia tatu katika shule ya Msingi Nyamalunda kata ya Kagunga Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wanalazimika kusoma wakiwa wamekaa chini kutokana na shule hiyo kukabiliwa na upungufu wa madawati kwa muda mrefu.
Changamoto hiyo imeibuliwa katika ziara ya kamati ya Sekretarieti ya chama cha mapinduzi (CCM) Wilayani Sengerema baada ya kutembelea shuleni hapo na kukuta wanafunzi wanasoma wakiwa wamekaa chini.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamesema kuwa wanasoma katika mazingira magumu na kwamba muda mwingine hushindwa kuelewa wanachofundishwa na walimu.
Mwalimu wa taaaluma katika shule ya Msingi Nyamalunda Mwl. Masunga Kulwa amesema kuwa changamoto hiyo imedumu kwa muda mrefu bila kutatuliwa .
Kufuatia hali hiyo katibu wa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Sengerema Jmal Athumani amelazimika kumpigia simu Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Binuru Shekidele na kuahidi kushughulikia changamoto hiyo.