Makala maalum ya siku ya Redio Duniani
13 February 2024, 12:18 pm
Redio Sengerema ni miongoni mwa redio za kijamii zaidi ya 30 zilizopo nchini Tanzania ambayo inapatikana katika mkoa wa Mwanza wilaya ya Sengerema. Tangu kuanzishwa kwake zaidi ya miaka 20 iliyopita imekuwa na mchango mkubwa sana kwa jamii ya wakazi wa Kanda ya Ziwa wakiwemo wavuvi, wakulima na wafugaji pamoja na wachimbaji wanaopatikana katika maeneo hayo.
Pamoja na kuwa na mchango baado Jamii ya Sengerema imekuwa ikitumia Radio kutoa elimu na taarifa mbalimbali kama inavyojipambanua kwa kauli mbiu yake ya “Chemchemi ya Maarifa” na hii ni baadhi tu ya mchango wake katika jamii, ikiwa leo ni Siku ya Radio Dunia kwa mwaka huu 2024 iliyobebwa na kauli mbiu isemayo “KARNE YA KUFAHAMISHA,KUBURUDISHA NA KUELIMISHA”