Wananchi walia kutelekezwa eneo la stend Sengerema
1 November 2023, 5:20 pm
Ikumbukwe kuwa kwenye mkutano wa Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh. Senyi Ngaga uliofanyika katika eneo la ujenzi wa shule ya sekondari Nyampulukano mwezi Mei mwaka huu ,Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Sengerema Binuru Shekidele aliwaahidi wananachi kuwa stendi hiyo itarejeshwa mwezi Julai mwaka huu ambapo mpaka sasa hakuna kinachoendelea kwenye eneo hilo.
Na:Emmanuel Twimanye.
Wananchi mtaa wa Mnadani kata ya Nyampulukano Sengerema mkoani Mwanza wamemlalamikia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Binuru Shekidele kwa madai ya kuchelewa kutekeleza ahadi ya kurejesha stendi ya magari madogo ya Mwembeyanga.
Wakizungumza na Radio Sengerema baadhi ya wananachi katika eneo la stendi hiyo wamesema kuwa licha ya Mkurugenzi mtendaji kuwaahidi kuirejesha stendi hiyo mwezi Julai mwaka huu lakini mpaka sasa hakuna utekelezaji wowote .
Katibu wa Mwenyekiti wa mtaa wa Mnadani Peter Ndimila amekiri kutorejeshwa kwa stendi hiyo hadi sasa na kuiomba serikali kufanya haraka mchakato wa kuirejesha ili kuchochea uchumi wa wanachi wa eneo hilo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya wilaya ya Sengerema Binuru Shekidele amesema kuwa wanasubiri kukaa kikao kwa ajili ya kupata hatima ya stendi hiyo.