Mkurugenzi aamuru wafanyabiashara kuondoka kando ya barabara
4 July 2023, 11:17 am
Kutokana na wafanyabiashara mjini Sengerema kuendesha shughuli zao pembezoni mwa barabara na kupelekea hofu ya kutokea ajali, hali hiyo imemuibua mkurugenzi wa halmashauri hiyo na kutoa siku tatu kwa wafanyabiashara hao kuondoka maeneo hayo .
Na: Said Mahera
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Sengerema mkoani Mwanza ametoa siku 3 kwa wafanyabiashara wa matunda wanaouza pembezoni mwa barabara mjini Sengerema kuondoka mara moja na kuhamia soko kuu kwa ajili ya kufanya biashara zao.
Mh Binuru Shehkidele amewataka wafanyabiashara kuondoka katika maeneo hayo kwani yanahatarisha maisha yao.
Akizungumza na wafanyabiashara hao baada ya kufanya ziara katika eneo wanaouza matunda mkurungenzi wa halmashauri ya Sengerema Mh. Binuru Shehkidele amewataka wafanyabiashara kuondoka katika maeneo hayo kwani yanahatarisha maisha yao.
Kwa upande wao wafanyabiashara wa matunda wamesema kuwa kuhamishwa katika sehemu hiyo na kupelekwa katika soko kuu itapelekea maisha yao kuwa magumu kutokana na ugumu watakaoupata katika soko hilo.
Hata hivyo mkurungezi huyo amewaomba viongozi wa wafanyabiashara wa matunda kama mjini Sengerema hawataridhika na sehemu hiyo wakae na wafanyabiashara hao na kupendekeza maeneo ambayo ni rafiki kwao lakini isiwe maeneo ya barabarani.
Kwa upande wake mwenyekiti wa soko kuu Bwn. Semeni Manoti amesema maeneo ya kufanyia biashara yapo na kuwaomba wafanyabiashara wa matunda kuzingatia agizo la mkurungezi huku akiwaondoa wasiswasi muda wa kufunga soko hilo.
Suala la kuhamisha wafanyabiashara wa matunda katika maeneo ya pembezoni limekuwa likifanyika kila mara na wafanyabiashara hao kurudi katika maeneo hayo.