Simba Sc kupigania point3 Misungwi, kukaa kileleni mwa Ligi kuu VPL
23 April 2021, 8:50 pm
Kocha msaidizi wa Simba sc Suleiman Matola amesema katika metch yao dhiidi ya Gwambina fc ya jijini Mwanza utakao chezwa hapo kesho katika uwanja wa Gwambina Misungwi utawahakikishia kuanza kukaa kileleni mwa ligi kuu Tanzania bara.
Akizungumza wa wandishi wa habari kocha Matola amesema wanaiheshimu sana Gwambina Fc hasa inapokuwa katika uwanja wao wa Nyumbani Misungwi imekuwa ikifanya vizuri, japo kwa metch ya Simba sc itahakikisha inaondoka na point zote 3 na kujikusanyia point 9 kanda ya Ziwa.
Kwa upande wake kocha wa Klabu ya Soka ya Gwambinafc Mohamed Badk amesema wataiheshimu Simba katika mchezo huo kama team kumbwa inayo shiriki klabu bingwa Afrika na kuwa bingwa mtetezi wa ligi kuu Tanzania hivyo watahakikisha wanazitetea point 3 katika uwanja wa nyumbani ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.
Nao manahoza wa vilabu hivyo wamesema walimu wao wamewafundisha vizuri hivyo watatumia uzoefu huo kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi katika mchezo huo.
Shirikisho la Mpira wa miguu Mwana MZFA limetangaza kingilio katika mchezo huo ambapo kwa mzunguko ni sh.8,000/= vip B sh.15000/= na vip A ni sh.20,000/=