Bank ya CRDB Sengerema yatoa mifuko 100 ya saruji kujenga shule ya sekondari.
15 April 2021, 9:32 am
Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza Dr.Emmanuel Kipole amepokea mifuko mia moja ya saruji kutoka Bank ya Crdb kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya wasichana wilayani hapo.
Akizungumza baada ya kukabidhi saruji hiyo Manager biarashara wa Crdb Bank kanda ya magharibi Bwn, Jumanne wagana amesema wametoa mifuko 100 ya saruji yenye thamani ya shiringi milian 2/= kwa lengo la kuunga juhudi za viongozi wa wilaya hiyo za kuinua sekta ya elimu hasa kwa watoto wa kike.
Naye manager wa CRDB Sengerema Bi.Rose nombo amewataka wananchi kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu huku akiwaomba kushirikiana na Bank hiyo katika huduma mbalimbali za kijamii na za kifedha.
Kwa upande wake mkuu wilaya ya Sengerema Dr. Emmanuel Kipole ameishukuru benk ya Crdb kwa kujitoa saruji hiyo ambayo itawezesha kuanza kwa ujenzi wa shule mpya ili kuongeza wigo wa elimu wilwyani hapo.
Halmashauri ya wilaya ya Sengerema inatarajia kujenga shule mpya kumi kwa lengo la kupunguza mrundikano wa wanafunzi madarasani na mojawapo kati hizo ni shule ya kidato cha tano na sita ya wasichana pekee itakayo jengwa katika kata ya mission wilayani hapo.
Zaidi sikiriza sauti za viongozi hao wakati wa makabidhiano………