Zao la alizeti latajwa kunyanyua uchumi wa wananchi Sengerema
6 April 2021, 6:14 pm
Afisa kilimo kata ya Nyatukala Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza Bi. Jonesia Joseph amewataka wakazi wa kata hiyo kutumia mvua zinazoendelea kunyesha katika kilimo ili kujipati chakula pamoja na kipato.
Bi Jonesia ametoa kauli hiyo ofisini kwake nakusema kuwa kutokana na aridhi kuwa na kiasi kikubwa cha maji kwasasa hivyo wakulima wanapaswa kulima mazao ya muda mfupi kama vile viazi na mtama ili kuondokana na upungufu wachakula.
Aidha afisa kilimo huyo amewaasa wakulima kutumia maafisa ugani walioko katika kila semu katani humo ili kupewac elimu jinsi ya kujihusisha na kilimo cha alizeti ambacho ni cha mkakati kwa lengo la kujipatia kipato kupitia zao hilo.
Kata ya Nyatukala hujihusisha zaidi na kilimo cha mazao ya chakula kama mahindi,nyanya na viazi hivyo ni vyema pia wakulima kujihusisha na zao la alizeti ili kupata maligafi kwaajili ya viwanda ili kujikwamua kiuchumi.