Rais Mama Samia atoa maagizo mazito kwa TAKUKURU
28 March 2021, 1:28 pm
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuharakisha kesi, kuondoa kesi sizizo na msingi na za kubambikiwa ili kuondokana na idadi kubwa ya kesi ambazo Serikali inashindwa.
Rais Samia ameyasema hayo leo Jumapili, Machi 28, 2021 baada ya kupokea ripoti ya (CAG) na (TAKUKURU) Ikulu ya Chamwino, Dodoma.
Amesema amefurahishwa kusikia tathmini ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa kiwango cha asilimia 89.8 ya malengo yaliyopangwa hivyo kuitaka ijipime zaidi na kuongeza juhudi hasa katika kuharakisha kesi.
Rais Samia ameitaka Takukuru kuendelea kuzisimamia zile zenye uhalali kwa kuzifanyia kazi kwa kasi na kuzifikisha kunakotakiwa, huku ikipunguza idadi ya kesi ambazo wanashindwa mahakamani.
“Hapa kuna kesi tunazoshindwa na hizi hazikuwa na misingi mizuri au zilikuwa za kubambikizwa yote yapo haya! Kwa hiyo nakuomba Mkurugenzi zile ambazo huna misingi mizito ya kuweza kushinda zifute kabla hujazipeleka huko kila siku kusema kuna kesi tumeshindwa hazina tija kwa Serikali.