Orkonerei FM
Orkonerei FM
1 June 2025, 11:37 am
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limefanya ukaguzi maalumu wa mabasi ya abiria ili kudhibiti ajali kutokana na ongezeko la wasafiri kipindi cha likizo za shule. Madereva wamehimizwa kuzingatia sheria za barabarani huku abiria wakitakiwa kununua tiketi kwenye ofisi rasmi…
30 May 2025, 2:56 pm
Jeshi la Polisi limeendesha mafunzo kwa madereva 800 wa magari ya utalii Arusha, kuelekea msimu wa utalii ili kuhakikisha sheria za barabarani zinafuatwa na usalama wa watalii unaimarishwa. Na Nyangusi Ole Sang’ida Zaidi ya madereva 800 wa magari ya utalii…
26 May 2025, 6:47 pm
“Kilichotokea ni mauaji, inaelezwa kwamba walikuwa baa, baada ya kuwa baa nadhani ugomvi ulitokea, wakapigana. Akachukuliwa akaenda kufia hospitalini. Vijana wengine kutoka kule anakotoka marehemu walikuja kuchoma moto nyumba ya mtuhumiwa na kuharibu migomba iliyokuwa karibu na nyumba hiyo,” amesema…
26 May 2025, 10:19 am
“Serikali yetu haiwezi kufurahia kuona jamii yetu inahangaika na masuala ya malisho. Nimejiridhisha kwamba maeneo yetu yataendelea kutumika kwa malisho na mafunzo ya kijeshi,” alisema Lowassa. Na Nyangusi Ole Sang’ida Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mhe. Fredrick Lowassa amewataka wananchi…
25 May 2025, 9:50 am
Na Nyangusi Ole Sang’ida Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha limetoa mafunzo maalumu kwa madereva wanaoendesha magari ya Serikali mkoani humo, ili kuwajengea uwezo wa matumizi sahihi ya barabara na mifumo mipya ya Jeshi hilo. Akizungumza…
18 May 2025, 2:46 pm
“Kwakweli ushirikiano huu ni muhimu sana kwani sisi wafugaji bila kuwa na mazingira bora, maisha yetu na mifugo yetu yatakuwa hatarini. Pia kwa kushirikiana tutaweza kupata fedha zaidi kutoka kwa wafadhili na kutumia rasilimali zetu kwa ufanisi zaidi kufikia maeneo…
17 May 2025, 12:00 pm
Nijuze Radio Show Katika toleo hili maalum la Nijuze Radio Show, Dorcas Charles na Isack Dickson wanatembelea kata ya Endiamtu, ndani ya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mirerani Simanjiro mji wa Tanzanite, ndoto, vijana na harakati. Kipindi kinachunguza kwa undani…
17 May 2025, 10:13 am
Mama Lishe na Baba Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia majiko ya gesi bure, wakisema yatapunguza madhara ya kiafya na kulinda mazingira. Viongozi wa halmashauri hiyo wamesema hatua hiyo inalenga kuondoa…
15 May 2025, 3:03 pm
“Huu ndiyo wakati wa kuhakikisha maeneo yetu ya malisho yanalindwa, kuhifadhi mbegu za majani, na kuhakikisha tunafuata utaratibu wa kulisha mifugo ili kipindi cha ukame kisitukute hatuna maandalizi,” Kone Medukenya Na Baraka David Ole Maiaka Jamii ya wafugaji wa kijiji…
12 May 2025, 11:39 am
“Niliamka tu asubuhi nikawa ninajisikia vibaya nikaamua kwenda duka la dawa kununuwa dawa za malaria…kumbe ilikuwa UTI” Bi Fatuma Na Isack Dickson Aliamka asubuhi akiwa na maumivu ya kichwa, Akaenda duka la dawa, akaeleza dalili, na kupewa dawa. Bila vipimo,…
DIRA:
Kuwa na jamii ya kifugaji yenye uelewa na ufahamu mpana katika maendeleo kupitia upashanaji wa habari
DHAMIRA:
Kuandaa na kurusha vipindi vya kuboresha maisha ya jamii katika elimu, afya, usawa, uongozi na utawala Bora.
Orkonerei FM Redio ni Redio ya jamii iliyopo katika kijiji cha Terrat wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara iliyoanzishwa mwaka 2002 kwa lengo la kuelimisha, Kuhabarisha na kuburudisha jamii za wafugaji na jamii zingine zilizopo katika mkoa wa Manyara,Arusha,Kilimanjaro na mkoa wa Tanga.
Orkonerei FM Redio inapatikana kwa masafa ya 94.3 MHz na kauli mbiu yetu ni “Sauti yako,Sauti ya jamii”