Orkonerei FM

Wanawake na kilimo cha nyasi zinazostahimili ukame kama mbinu ya kuukabili ukame

12 February 2026, 3:44 pm

Pichani ni akina mama wa kikundi cha Eramatare kijiji cha Terrat wilaya ya Simanjiro katika shamba darasa la kupanda na kuvuna nyasi kwaajili ya mifugo kijiji cha Terrat.

Na Isack Dickson

Katika wilaya ya Simanjiro, mabadiliko ya tabianchi yamesababisha vifo vya zaidi ya mifugo 92,000 kwa mwaka mmoja pekee,lakini katikati ya changamoto hiyo, kundi la wanawake mashujaa, kwa msaada wa Baraza la Wanawake Wafugaji (PWC) na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali, wamepata mbinu mpya ya kujiokoa: kilimo cha nyasi zinazostahimili ukame.

Makala hii ya kusisimua inakupeleka hadi Simanjiro kusikia sauti za wanawake walioacha kuwa wahanga na kuwa wafanyabiashara wa nyasi, wakiongeza kipato cha familia na kupunguza vifo vya mifugo kwa asilimia 30. Pata uchambuzi wa kina kutoka kwa wataalamu wa mifugo na sayansi ya tabianchi kuhusu jinsi mradi huu unavyoendana na Agenda 2063 ya Umoja wa Afrika na malengo ya kimataifa ya maendeleo endelevu (SDGs).

Makala kamili kwa Sauti.