Orkonerei FM

Tujitokeze kuboresha taarifa zetu tuwe na sifa za kupiga kura

24 September 2024, 7:16 pm

Mkuu wa mkoa wa Manyara Mh.Queen Cuthbert Sendiga akihutubia katika mkutano wa hadhara kijiji cha terrat wilaya ya simanjiro ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku tano katika wilaya ya Simanjiro. (Picha na Evanda Barnaba)

Na Dorcas Charles

Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwaka 2025 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh.Queen Sendiga amewataka wananchi wa Kata ya Terrat kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura kuanzia tarehe 25 mpaka tarehe 01 oktoba mwaka huu.

Mkuu wa mkoa Sendiga ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Terrat katika ziara yake katika Wilaya ya Simanjiro leo tarehe 24.9.2024 pia amewasihi kujitokeza kuwania nafasi za uongozi wa serikali za mitaa ambapo uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika terehe 27.11.2024.