Orkonerei FM
Wanajamii wapewa elimu juu ya kujiingizia kipato kipindi cha ukame
9 July 2024, 1:35 pm
Na Joyce Elias.
Afisa kilimo kata ya Terrat Ndg.PETRO MEJOOLI LUKUMAY amesema kuwa wanajamii wanatakiwa kulima mbogamboga na mazao mengine mchanganyiko ili kujiingizia kipato haswa wakati wa upungufu wa mvua ama ukame.
Ametoa elimu hiyo kupitia mahojiano mafupi aliyoyafanya na mwandishi wetu JOYCE ELIUS, ambapo amesema kuwa wao kama wataalamu huwa wanapata nafasi katika mikutano ya kijamii kutoa elimu hizo ili kupambana na ukame wakati wanajamii wanajiingizia kipato.