Nini kinawakwamisha vijana kushiriki kuwania nafasi za uongozi?
24 May 2024, 12:13 pm
vijana wa kijiji cha Terrat wakitumbuiza kwenye mkutano (picha na Isack Dickson)
“Kutokana na kipato kidogo vijana hawana hela za kuweza kuwawezesha kwenye michakato ya uchaguzi” Kijana.
Na Dorcas Charles
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 vijana ni asilimia 46. Tafsiri ya kijana inasema kijana ni yule mwenye umri wa miaka 15 hadi 35
Sera ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2019 inataka ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika ngazi zote za maamuzi mjini na vijijini
mkakati wa sera ya vijana umeainisha bayana majukumu ya kila mdau katika kufanikisha sera ya maendeleo ya vijana ili kufikia malengo ya kuwawezesha vijana nchini katika nyanja za kiuchumi ,kijamii na kisiasa
Lakini jee malengo haya yanaakisi na sera inavyoseama, Vijana wanaeleza nini kinapelekea wao kutokushika nafasi za uongozi?
Sauti ya baadhi ya bijana kutoka mkoani Arusha
Inatambulika kuwa vijana ndio wenye nguvu , wazalishaji na wakati mwengine enye ubunifu na afya na ni kundi kubwa lililopo katika jamii swali la kujiuliza wanaaminika katika kushika nafasi za uongozi, baadhi ya wazee wa mtaa wa mita 200 kata ya Ngarenaro mkoani Arusha wanaeleza
Sauti ya baadhi ya wazee Mkoani Arusha
Ili kuhakikisha masuala yanayowakabili vijana yanashuhulikiwa ni muhimu kuwa na makakati wa kuwashirikisha vijana katika mchakato wa maamuzi na majukumu ya uongozi na kuwaandaa vijana katika nafasi za uongozi
Wenyekiti wa mtaa wa Mita mia mbili Kata ya Ngarenaro Jijini Arusha Peter Lukumay anasema wao wanawaanda vjana kushika nafasi za uongozi
Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji cha Mita mia mbili
Ili vijana wengi kujitokeza kuwania nafasi za uongozi katika chaguzi zote za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu nini kifanyike, vijana hawa na mwenyekiti wa kijiji cha mita 200 wanaeleza
Sauti ya baadhi ya vijana na mwenyekiti wa Mita Mia mbili mkoani Arusha