Sengerema FM

Achomwa moto mpaka kufa kisa debe tatu za mpunga

30 May 2024, 8:30 am

Eneo alilochomwa mwizi wa mpunga na wananchi wenye hasira kali kitongoji cha Kanyele -Picha na Emmanuel Twimanye

Matukio ya vijana kujihusisha na wizi yamekuwa yakitajwa kushamili hasa kwa maeneo ya vijijini wilayani Sengerema kutokana wananchi wengi kuvuna mazao ambapo chanzo chake kinadaiwa kuwa baadhi ya vijana kujihusisha na michezo ya kamali bila chanzo kingine cha kipato.

Na:Emmanuel Twimanye

Kijana mmoja ambaye hajafahamika jina lake amedaiwa kuuawa kwa kuchomwa moto  na watu wasiojulikana  kwa madai ya kuiba mpunga katika kitongoji cha Kanyele Kijiji cha Kang’hwashi  Kata ya Nyamizeze Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza .

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wananachi wamesikitishwa na tukio hilo na kuwaomba vijana kuachana na vitendo vya wizi. 

Sauti za wananchi wa kazi wa Nyamizeze

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kanyele Mathayo Kimoga Lyaloka  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo  huku akiwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.

Sauti ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kanyele Mathayo Kimoga Lyaloka

Naye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Senyi Ngaga ameitahadharisha jamii kuachana na tabia ya  wizi  badala yake wafanya kazi halali zitakazowasaidia kujipatia kipato.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Senyi Ngaga