Sengerema: Watakaofanya uhalifu sikukuu za Pasaka kukiona
29 March 2024, 6:41 pm
Wakristo ulimwenguni kote wanaungana kuadhimisha sikukuu ya Pasaka kama kumbukumbu ya mateso, kufa na kufufuka kwa bwana Yesu kristo.
Na;Emmanuel Twimanye
Serikali ya mtaa wa Geita Road kata ya Nyatukala wilayani Sengerema mkoani Mwanza imetangaza mapambano makali dhidi ya wahalifu watakaothubutu kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika sikukuu ya pasaka .
Tamko hilo limetolewa na Mwenyekiti wa mtaa wa Geita Road Pelana Bagume kuelekea siku kuu ya pasaka na kusema kuwa Serikali ya mtaa huo wamejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na jeshi la polisi kufanya doria ili kukabiliana na wahalifu .
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amemewaomba wananchi kusherehekea siku kuu ya pasaka huku wakilinda mali zao nyumbani Ili kuepuka kuibiwa .
Nao baadhi ya wananchi wa mtaa huo wameahidi kutekeleza ushauri wa Mwenyekiti ikiwa ni pamoja na kusherehekea siku kuu ya pasaka kwa amani na utulivu huku wakilinda mali zao.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni watu wasiojulikana walivamia na kuvunja milango katika baadhi ya kaya mtaa wa Geita Road na kuiba mali mbalimbali za wananchi ikiwemo Fedha ,magodoro na Luninga kisha kutokomea kusikojulikana.