CCM Sengerema yaagiza kukamatwa fundi wa nyumba za walimu
13 February 2024, 5:09 pm
Kamati ya Sekretarieti ya ccm Wilaya ya Sengerema inafanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serkali ya awamu ya Sita, ambapo imekutana na changamoto ya Fundi aliyelipwa fedha na kushindwa kukamilisha majengo ya watumishi kisha kutokomea kusiko julikana.
Na:Emmanuel Twimanye
Wajumbe wa kamati ya Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza imeagiza kukamatwa fundi anayejenga nyumba za watumishi katika kata ya Nyamazugo Wilayani Sengerema Mussa Ntobi kwa madai ya kutelekeza ujenzi huo na kutokomea kusikujulikana.
Kamati hiyo imetoa agizo hilo baada ya kutembelea na kukagua Mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi katika kata hiyo unaojengwa kwa fedha za mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) na kukuta ujenzi umesimama , huku fundi akidaiwa kutokomea kusikojulikana na kupelekea kukwamisha ujenzi huo.
Kufuatia hali hiyo kamati hiyo imelazimika kumpigia simu Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema anayesimamia mradi huo Elias Mwita ili kujua nini kimekwamisha ujenzi huo .
Diwani wa kata ya Nyamazugo Mh,Enock Sengerema na afisa mtendaji wa kata hiyo Elikana Ndiganya wameahidi kutekeleza maagizo ya kamati ya sekretarieti.
Katika hatua nyingine kamati hiyo imeshauri mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Sengerema Binuru Shekidele kumwondoa afisa mtendaji wa kata ya Nyamazugo katika katya hiyo Elikana Ndiganya kwa madai ya kushindwa kutimiza majukumu yake .
Aidha kamati ya Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi Wilayani Sengerema imetembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika kata ya Nyamazugo ,Kasungamile pamoja na mradi wa ujenzi wa Bweni la wasichana katika kata ya Nyamatongo.