Sengerema waadhimisha miaka 62 ya uhuru kwa kufanya usafi wa mazingira
9 December 2023, 7:36 pm
Maadhimisho ya kumbukizi ya kutimiza miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania bara wilayani Sengerema yamefanyika kwa kupanda miti na kufanya usafi maeneo mbalimbali, huku wananchi wakitakiwa kudumisha Umoja na mshikamano kama chachu ya maendeleo ya taifa.
Na Emmanuel Twimanye.
Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Mkoani mwanza imeadhimisha miaka 62 ya uhuru wa Tanzania bara kwa kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Wilaya ya Sengerema , Kituo cha afya Sengerema pamoja na kupamba miti Zaidi ya Elfu moja katika maeneo mbalimbali .
Akizungumza baada ya zoezi hilo katibu tawala wa Wilaya ya Sengerema Cathbert Midala amewashukuru wananachi na viongozi mbalimbali waliojitokeza kufanya usafi katika na kuwataka kuendelea kutunza mazingira kwa kijazi cha sasa na kijacho.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Binuru Shekidele amesema kuwa wameamua kuadhimisha miaka 62 ya uhuru wa Tanzania bara kwa vitendo ili kuenzi uhuru huo.
Mgamga mkuu wa Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Dkt Fedrick Mgalula amewashukru wananchi na viongozi mbalimbali wa serikali kwa kufanya usafi katika Hospitali hiyo ili kutunza mazingira.
Nao baadhi ya wananachi waliojitokeza kufanya usafi wamesema kuwa wameamua kufanya usafi ili kuunga mkono jitihada za serikali za kutunza mazingira.
Aidha Tanzania bara ilipata uhuru Desemba 9 mwaka 1961, kutoka kwa Waingereza .