Wazazi watakiwa kufuatilia mienendo na malezi ya watoto wao
31 October 2023, 8:55 pm
Wazazi na walezi wilayani Sengerema mkoani Mwanza wanatajwa kujali zaidi shughuri zao binafsi na kuonyesha kulitegea mgongo suala la malezi kwa watoto, huku wenginge wakiwaachia watoto kuwalea watoto wenzao.
Na:Emmanuel Twimanye.
Wazazi Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wametakiwa kutimiza jukumu la malezi ya watoto badala ya kuwacha watoto wajilee wenyewe hali inayohatarisha usalama wa maisha yao.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Dawati la Jinsia na watoto kutoka jeshi la polis Wilayani Sengerema Mponela Malongo kufuatia baadhi ya wazazi kushindwa kutimiza jukumu la malezi kwa watoto na kusema kuwa jukumu la kulea watoto ni la mzazi na si mtoto.
Katika hatua nyingine ameiomba jamii kuacha kuficha matukio ya ukatili pindi wanapofanyiwa watoto kwa madai ya kulipwa fedha na wahusika kwa kuwa hali hiyo inamwathiri mtoto.
Nao baadhi ya wazazi wamekiri kutotekeleza suala la malezi kwa watoto kwa madai ya kujikita katika shughuli za kutafuta kipato cha familia.