Waziri Makamba atoa ahadi hii kwa wananchi Sengerema
16 July 2022, 3:55 pm
Waziri wa Nishati Nchini Mh,January Makamba amewahidi wananchi Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza kutatua tatizo sugu la kukatika kwa umeme ili kuwaondolea adha hiyo inayowakabili kwa muda mrefu .
Waziri Makamba amesema hayo wakati akizungumza na wananachi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kituo cha zamani cha mabasi wilayani humo.
Amesema kuwa Serikali itajenga njia ya pili ya umeme kutoka Mkoani Geita ambapo zoezi hilo linatarajia kukamilika mwezi Oktoba pamoja na kujenga njia nyingine kubwa zaidi ambayo itakwenda kwenye mgodi wa Nyanzaga .
Naye Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mh,Hamis Tabasam amemshukru waziri huyo wa nishati kwa kutembelea katika jimbo lake na kujionea namna wananachi wanavyokabiliwa na tatizo la kukatika kwa umeme na kutoa maagizo kwa mamlaka husika wilayani humo.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wilayani humo wamesema kuwa kero ya kukatika kwa umeme inarudisha nyuma maendeleo yao na wilaya kwa ujumla.
.