Kuelekea miaka 63 ya uhuru Sengerema yafanya usafi hospitali ya wilaya
8 December 2024, 10:14 pm
Hivi karibuni waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alielekeza maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania yafanyike Kwa ngazi za Mikoa na Wilaya, kwa kufanya shughuli za kijamii zikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira katika maeneo ya kijamii kama vile hospitali, masoko, kambi za wazee na wenye uhitaji maalumu.
Na;Elisha Magege
Kuelekea miaka 63 ya uhuru wa Tanzania bara, Halmashauri ya Sengerema imefanya usafi katika hospitali ya wilaya Mwabaruhi na kituo cha afya Sengerema.
Akizungumza baada ya zoezi hilo katibu tawala wilaya ya Sengerema Bwn. Cuthibert Midara amesema wilaya ya sengerema mwaka huu inaazimisha miaka 63 ya uhuru kwa kufanya usafi maeneo mbalimbali pamoja na kupanda miti kama kumbukumbu ya maadhimisho hayo.
Naye Kaimu mkurugenzi Halmashauri ya Sengerema Wilbert Bandola amewashukuru wananchi na viongozi walio jitokeza leo kufanya usafi katika maeneo ya hospitali licha ya kuwa ni siku ya pumziko.
Aidha Afsa usafishaji na udhibiti wa taka ngumu mjini Sengerema Bi.Ester Lucas na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali waliojitokeza kufanya usafi siku ya wamewashukuru viongozi wa wilaya kwa kuteua maeneo ya huduma za afya kufanya usafi.