Sengerema FM

DC Sengerema aongoza wananchi kujiandikisha kushiriki uchaguzi

12 October 2024, 4:23 pm

Mkuu wa wilaya ya Sengerema akijiandikisha kwenye daftari la mpiga kura. Picha na Emmanuel Twimanye

Serkali kupitia TAMISEMI imetangaza siku kumi za wananchi kujiandikisha kwenye daftari la makazi kwa ajili ya kushiriki uchaguzi serkali za mitaa mwezi november mwaka huu.

Na.Emmanuel Twimanye

Wananachi Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wametakiwa kuendelea kujitokeza  kujiandikisha katika Daftari la makazi kwa ajili ya kushiriki  uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Senyi Nganga wakati  akijiandikisha  katika daftari la wapiga kura katika kituo cha Shule ya msingi Kilabela na kusema kuwa wananachi hawanabudi kuendelea kujitokeza kujiandikisha ili wapate nafasi ya kushiriki uchaguzi  huo.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Senyi Nganga akiwahimiza wananchi kujiandikisha

Katika hatua nyingine  Mkuu wa wilaya amewaomba wananachi kutochanganya zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na zoezi lililopita la kuboresha kitambulisho cha mpiga kura kwani kitambulisho hicho kinatumika kwenye uchaguzi mkuu, na  kwa wananachi watakaojiandikisha katika daftari la sasa  la makazi  ndio watakaoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.  

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Senyi Nganga akizungumzia changamoto za baadhi ya wananchi kushindwa kutofautisha kitambulisho cha mpiga kura na daftari la mpiga kura

Aidha uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu .