Sengerema FM

Faustine akutwa amejinyonga chumbani kwake Sengerema

11 September 2024, 8:12 pm

Picha ya kamba ya kitanzi kutoka Mtandaoni

Matukio ya vijana kujinyonga wilayani Sengerema yanazidi kushika kasi huku chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi na ugumu wa maisha.

Na;Emmanuel Twimanye

Kijana  mwenye umri wa miaka 34 aliyefahamika kwa jina la Faustine Malima amefariki Dunia kwa kujinyonga  chumbani kwake katika Kitongoji cha Misheni Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza ,huku chanzo cha tukio hilo kikiwa bado hakijafahamika.

Akizungumzia tukio hilo  Magdalena Malima  ambaye ni mdogo wake na marehemu amesema kuwa  alipigiwa simu na mama yake akihitaji kuongea na Faustine na kumwagiza  mtoto wake ampelekee simu ndani ndipo alipokuta amejinyonga na kupoteza maisha.

Sauti ya Magdalena Malima  mdogo wake na marehemu

Baadhi ya majirani wa familia hiyo wamesikitishwa na tukio hilo na kuwaomba vijana kuacha kujichukulia  maamuzi magumu ya kujitoa uhai.

Sauti ya Majirani wakizungumzia tukio la kijana kujinyonga

Mwenyekiti wa kitongoji cha Misheni Joseph Protas  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limetokea leo majira ya saa  tatu  asubuhi na kuwataka vijana kuwashirikisha ndugu pindi wanapokutana na changamoto za maisha na si kuchukua maamuzi ya kujinyonga.

Sauti ya mwenyekiti wa kitongoji cha Misheni Joseph Protas akizungumzia tukio la kijana kujinyonga

Aidha Jeshi la Polisi  Wilayani Sengerema limefika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kisha kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema.