Sengerema FM

Mwanafunzi adakwa na polisi jamii akiiba simu chuoni Sengerema

10 September 2024, 5:50 pm

Mwanafunzi anayetuhumiwa kuiba simu Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Sengerema akiwa kwenye gari kuelekea kituo cha polisi Sengerema.Picha na Emmanuel Twimanye

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Sengerema (FDC) ni miongoni mwa vyuo vikongwe nchini vya maendeleo ya wananchi na kimekuwa kikipokea wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Na:Emmanuel Twimanye

Mwanafunzi wa chuo cha Maendeleo ya Wananachi Sengerema (FDC) kilichopo wilayani Sengerema mkoani Mwanza  amekamatwa na Polisi Jamii kata ya Nyampulukano kwa tuhuma za kuvamia na kuiba simu za wanachuo wenzake  katika chuo hicho .

Akizungumza  akiwa  chini ya ulinzi wa  polisi jamii  Paul  Samwel  mwanafunzi  anayetuhumiwa kuiba simu za wenzake  amekiri kuiba simu hizo.

Sauti ya Paul  Samwel  Mwanafunzi anaetuhumiwa kuvunja na kuiba simu

Baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho na wananchi wamesikitishwa na tukio hilo na kuiomba jamii kushirikiana kwa pamoja kukomesha matukio  hayo.

Sauti ya Baadhi ya wanafunzi na wananchi wakizungumzia tukio la wizi

Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya wananchi  (FDC) Wilayani Sengerema Monica Lukeha ameahidi kumfukuza chuo mwanafunzi huyo na kuwaomba wazazi kuendelea kuwafundisha watoto wao maadili mema .

Sauti ya mkuu wa chuo cha Maendeleo ya wananchi  (FDC) Wilayani Sengerema Monica Lukeha

Naye Kamanda mkuu wa Polisi jamii kata ya Nyampulukano Lenatus Lugadija Ngoma  amethibitisha  Jeshi hilo kumkamata mwanafunzi huyo  anayeishi nje ya  chuo  na kusema kuwa alivamia  chuoni hapo majira ya saa tisa usiku wa kuamkia leo na kuiba simu za wanachuo.

Sauti ya Kamanda mkuu wa Polisi jamii kata ya Nyampulukano Lenatus Lugadija Ngoma

Hata hivyo  Mwanafunzi huyo amefikishwa katika kituo cha Polisi Wilayani Sengerema kwa hatua zaidi.