Sengerema FM

Sotta mining yatoa mafunzo ya fulsa za kibiashara Sengerema

27 March 2026, 6:58 pm

Baadhi ya wafanyabiashara wakipokea mafunzo kutoka kwa Mhandisi mkuu wa mgodi wa Sotta

Kutokana na kuanzishwa kwa mgodi wa dhahabu Wilayani Sengerema, Kampuni ya Sotta mining imetoa mafunzo kwa wafanyabiashara ili kuzijua na kuzitumia fursa zilizopo mgodini

Na,Emmanuel Twimnye

Wafanyabiashara Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wameipongeza kampuni ya mgodi wa Sotta kwa kuwapatia mafunzo ya namna ya kuchangamkia fursa zitakazotokana na shughuli za mgodini, ikiwemo utaratibu wa kupata zabuni.

Wafanyabiashara hao wametoa pongezi hizo baada ya kupatiwa  mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Sengerema ambapo wamesema kuwa  wameelewa fursa zilizopo mgodini na namna ya kushiriki katika utoaji wa huduma na bidhaa, huku wakiahidi kuzitumia fursa hizo kujikwamua kiuchumi.

Sauti ya wafanyabiashara Sengerema

Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema wamepongeza hatua hiyo hatua hiyo  itasaidia kukuza biashara na  kuchochea  uchumi wa wilaya kwa ujumla.

Sauti za madiwani wa Halmashauri ya Sengerema

Mbunge wa Jimbo la Sengerema, Mh,Hamis Tabasam, amewahimiza wafanyabiashara kutumia vyema maarifa waliyopata ili wanufaike na fursa za uwekezaji wa mgodi huo.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Sengerema, Mh,Hamis Tabasam

Kwa upande wake, Mhandisi  mkuu wa kampuni ya mgodi wa Sotta, Richard Ojendo, amesema ujenzi wa mgodi unaendelea na unatarajiwa kuanza uzalishaji rasmi mwaka 2027.

Sauti ya Mhandisi mkuu mgodi wa Sotta Richard Ojendo