Sengerema FM
Sengerema FM
5 December 2025, 5:21 pm

Madiwani Halmashauri ya Sengerema wamekula kiapo cha kuwatukia wananchi wa Halmashauri hiyo baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oct.29 2025
Na,Emmanuel Twimanye
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza wamewatakiwa kwenda kufanya kazi kwa kutanguliza mbele maslahi ya wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Senyi Ngaga katika mkutano wa kwanza wa baraza la madiwani uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za Halmashauri ya wilaya hiyo uliokwenda sambamba na zoezi la kuapisha madiwani.
Awali wakiapishwa madiwani na Hakimu mfawidhi ya mahakama ya Wilaya ya Sengerema Evoid Kisoka wameapa kuitumikia Halmshauri ya wilaya ya Sengerema ,kulinda na kuitetea katika ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika kikao hicho, baraza hilo limemchagua Diwani wa kata ya Nyamatongo Yanga Makaga amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Halmshauri hiyo kwa kura 35 pamoja na makamu mwenyekiti wa Halmshauri hiyo Diwani wa kata ya Kahumulo Fortunatus Nzwagi kwa kura 35 ambapo matokeo hayo yametangazwa na katibu tawala wa wilaya ya Sengerema Cathbeth Midala.
Kwa upande wake Rose Mgasha kutoka Sekeretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya ziwa Mwanza,amewaomba madiwani kwenda kufanya kazi kwa uadilifu .
Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Binuru Shekidele amewaomba madiwani kuungana na kwenda kuwatumikia wananchi .

Naye Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Yanga Makaga amewashukuru madiwani kwa kuwamini na kumchagua ili awatumikie huku akiagiza Halmashauri hiyo kuhakikisha inaongeza mapato pamoja na kupunguza matumizi ya fedha yasiyokuwa ya lazima.
