Sengerema FM

Madiwani Buchosa waapa kumaliza Kero na Migogoro kwa wananchi

5 December 2025, 4:51 pm

Bi. Rose Mgasha wa Sekratalieti ya maadili kwa viongozi Kanda ya Ziwa akizungumza na madiwani wa Halmashauri ya Buchosa.Picha na Michael Mgozi

Madiwani wateule waapisha rasimi kuwatumikia wananchi baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Mwenzi Oktoba 29 2025 katika Halmashauri ya Buchosa mkoani Mwanza.

Na,Michael Mgozi

Madiwani na Watumishi wa Halmashauri ya Buchosa wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kupunguza migogoro na kero kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buchosa Mh.Isack Charles Mashimbamda mfupi baada ya kuchaguliwa na baraza la madiwani kwa kura 27 kati ya kura 28 katika ukumbi wa Halmashauri ya Buchosa Mkoani Mwanza, nakusema kuwa hatosita kupambana na watumishi wasio wajibika huku akiwataka kufanya kazi bila upendeleo na kuhakikisha wanahudumia wananchi kwa haki.

Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buchosa Mh.Isack Charles Mashimbamda

Kabla ya kumchagua mwenyekiti huyo, Jumla ya Madiwani 28 katika Halmashauri ya Buchosa Mkoani Mwanza wamekula kiapo cha uaminifu, huku madiwani wakiahidi kusimamia raslimali zote na kufanya kazi kwa bidii kwani buchosa ina vyanzo vingi vya mapato.

Sauti za Madiwani wa Halmashauri ya Buchosa

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Buchosa Eriki Shingo amesema kuwa kipaumbele chake ni kuhakikisha anaongeza mapato katika halmashauri na jimbo kwa ujumla, huku akimpongea Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo, Benson Mihayo kwa kufanikisha ukusanyaji mapato ya Halmashauri ya Buchosa.

Sauti ya Mbunge wa jimbo la Buchosa Eriki Shingo

Hata hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa Benison Mihayo amewapongeza madiwani kwa kuchaguliwa huku akiwaomba kufanya kazi kwa bidii ili kuiletea maendeleo Halmashauri ya Buchosa.

Sauti ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa Benison Mihayo

Jumla ya madiwani 28 wamekula kiapo, ambapo madiwani 7 ni waviti maalum na madiwani 21 nikutoka katika kata ambazo zilifanya Uchaguzi October 29 mwaka huu,huku kata moja ya Nyakasungwa ikitarajiwa kufanya Uchaguzi wa diwani mwezi Novemba mwaka huukufuatia kifo cha aliyekuwa mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia chama cha mapinduzi ccm.

Madiwani wa Halmashauri ya Buchosa wakila kiapo.Picha na Michael Mgozi