Sengerema FM

Mwili wa mwanamme waopolewa Bwawani mjini Sengerema

19 November 2025, 4:50 pm

Picha ya Muonekano wa Bwawa la maji lililopo mjini Sengerema.Picha na Said Mahera

Matukio ya watu kujiua wilayani Sengerema yanazidi kuripotiwa, huku chanzo kikiwa bado hakijulikani

Na.Said Mahera

Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa majina ya Deusdetith Babila mkazi wa mtaa wa geita road kata ya nyatukala amekutwa amefariki dunia katika bwawa liliopo mtaa wa mjini kati kata ya Ibisabageni Wilayani Sengerema huku chanzo cha tukio hilo kikiwa hakijafahamika.

Wakizungumza na radio sengerema baadhi ya mashuhuda wamesikitishwa na tukio hilo nakuziomba mamlaka husika kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

Sauti za baadhi ya mashuhuda wa tukio

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa mjini kati Shemsa Jumanne Mlewa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwaomba ndugu wa familia kuwa wavumiliu katika kipindi hiki wakati serikali ikiendelea kufanya uchunguzi dhidi ya tukio hilo.

Sauti ya Mwenyekiti mtaa wa mjini kati Sengerema

Hata hivyo mwenyekiti huyu ameeleza kuwa jeshi la polisi wilaya ya sengerema limefika eneo la tukio na kuuchua mwili wa marehemu kisha kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti hospipitali ya wilaya ya sengerema.