Sengerema FM
Sengerema FM
26 October 2025, 8:42 pm

Zaidi ya wasimamizi wakuu na wasaidizi wa vituo vya kupigia kura 1,950 wanatarajia kwenda kusimamia vituo 650 vya kupigia kura katika jimbo la Sengerema wamekura kiapo cha uadilifu ili kutekeleza jukumu la uchaguzi mkuu jimbo la Sengerema.
Na Mwandishi wetu
Wasimami wa vituo vya kupigia kura katika Jimbo la Sengerema Mkoani Mwanza wametakiwa kuzingatia kanuni ,miongozo na sheria za uchaguzi ili uchaguzi huo ufanyike kwa uhuru na haki.
Kauli hiyo imetolewa na msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Sengerema Ally Salim wakati akifungua mafuzo ya siku mbili kwa wasimamizi wa vituo na wasimizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura yaliyofanyika katika umbi wa shule ya sekondari Sengerema kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Rais,wabunge na madiwani .
Katika hatua nyingine amewaomba kujiepusha kuwa chanzo cha malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa kwa kushirikiana vyema na mawakala wa vyama hivyo watakaokuwepo kwenye vituo kwa mujibu wa sheria .
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameahidi kuzingatia kanunu ,miongozo na sheria za uchaguzi.
