Sengerema FM
Sengerema FM
22 October 2025, 6:51 pm

Kampeni kuelekea uchaguzi mkuu zinaendelea maeneo mbalimbali ya nchi ambapo wagombea watoa ahadi ili wachaguliwe october 29 2025
Na,Mwandishi wetu
Mgombea ubunge jimbo la Buchosa kwa chama cha Sauti ya umma (SAU) Bi.Consolatha Cleophance Mtalyantula ameahidi kutatua changamoto za barabara na afya kwa wananchi wa jimbo hilo endapo watampa ridhaa ya kuwaongoza.
Akizungumza katika mkutano wa Kampeni Bi.Consolatha Cleophance Mtalyantula amesema yuko tayari kuwatumikia wananbuchosa kwa hali na mali kwani kwa muda mrefu wamekua wakilia na changamoto ya miundombinu ya barabara licha ya kuwa na rasilimali nyingi za mistu,samaki na mazao ya kilimo.
Baadhi ya wananchi jimbo la Buchosa wamewataka wagombea watakao changuliwa na kushinda nafasi za uongozi za Udiwani,Ubunge na rais kutekeleza ahadi walizo waahidi wananchi kwa haraka na uwazi.
Ikiwa zimesalia siku takribani saba watanzania tuweze kuingia katika uchaguzi mkuu viongozi mbalimbali wa dini,mila na Serikali wanazidi kuwaomba watanzania kujitokeza kupiga kura kwa njia ya amani, ili kuilinda na kuiheshimisha tunu ya Amani iliyowekwa na wasisi wa taifa hili.