Sengerema FM
Sengerema FM
12 October 2025, 5:02 pm

Kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2025 chama cha CHAUMMA kimeendelea na kampeni zake za kusaka kura kwa wananchi, kwa kuelezea sera na irani ya chama hicho.
Na,Mwandishi wetu
Mgombea ubunge jimbo la Buchosa kupitia chama cha Ukombozi wa umma (CHAUMMA) Ester Fulano ameahidi kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo endapo watampa ridhaa ya kuwaongoza katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika October 29 2025.
Akizungumza na Radio Sengerema Fulano amesema jimbo la Buchosa limekuwa nyuma kimaendeleo kutokana na wabunge walioongoza jimbo hilo kwa muda mrefu kusahau majukumu yao wanapo fika bungeni.
Katika hatua nyingine Fulano amesema ipo haja kwa wananchi wa Buchosa kufanya mamzi sahihi ya kuchagua viongozi wanaotokana na Chaumma ili kuleta maendeleo kupitia rasilimali zilizopo katika jimbo hilo.
Aidha Fulano amewataka wananchi kujitokeza kwenye mikutano ya kampeni kusikiliza sera za chama hicho kwani wamejidhatiti kushughulikia changamoto za wananchi kupitia ilani yake.