Sengerema FM
Sengerema FM
5 August 2025, 12:18 pm

Ikiwa vyama vya siasa nchini vinaendelea na zoezi la kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali ikiwemo Udiwani,Ubunge na Urais Tume ya uchaguzi nayo inaendelea na zoezi la kuratibu wasimamizi wa uchaguzi nganzi za Kata na Jimbo.
Na;Emmanuel Twimanye
Wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya Kata Jimbo la Sengerema Mkoani Mwanza wametakiwa kuzingatia taratibu ,kanuni ,sheria na miongozo ya uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uhuru ,haki na amani.
Kauli hiyo imetolewa na Hakimu mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Sengerema Evoid Kisoka wakati akifungua mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata katika ukumbi wa shule ya Sekondari Sengerema yaliyokwenda sambamba na zoezi la kuwapisha wasimizi hao .
Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Sengerema Ally Salim amesema kuwa idadi ya washiriki wa mafunzo hayo yatakayodumu kwa muda wa siku tatu ni 52 kutoka katika kata 26 za Jimbo hilo huku akiwaomba kuzingatia mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo wamesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kusimamia uchaguzi kwa weledi ikiwa ni pamoja na kuzingatia taratibu ,kanuni ,sheria na miongozo ili ufanyike kwa utulivu na amani.
Aidha uchaguzi mkuu wa wabunge ,madiwani na Rais unatarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu nchini.
