Sengerema FM
Sengerema FM
30 July 2025, 10:05 am

Shirika la Under the Same sun kwa kushirikiana na tasisi ya Village of Hop (VOH) wamefanya kumbukizi ya kuwakumbuka watu wenye ualbino waliouawa na kukatwa viungo vyao nchini, tukio hilo limefanyika mjini Sengerema kwenye mnala wa nithamini ulio na majina ya wahanga wa matukio hayo.
Na,Emmanuel Twimanye
Serikali Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza imeahidi kuendelea kuimarisha ulinzi dhidi ya watu wenye ualbino ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali za kisheria watu watakaobainika kujihusisha na mauaji dhidi yao

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Senyi Ngaga katika kumbukizi ya kuwaenzi watu wenye ualbino waliouawa ,kujeruhiwa pamoja na makaburi yao kufukuliwa kufukuliwa Wilayani Sengerema.
Baadhi ya watu wenye ualbino wakiwemo waliowahi kushambuliwa wameiomba serikali kuendelea kuimarisha ulinzi dhidi yao.
Makamu mwenyekiti wa chama cha watu wenye ualbino Taifa Alfred Kapole ameiomba jamii kuhakikisha kila mmoja anakuwa balozi wa kupinga mauaji dhidi kundi hilo .
Rais na mwazilishi wa Shirika la Under the Same Sun kutoka nchini Canada Peter Ash amesema kuwa ndoto yake ni kuona siku moja watu wenye ualbino nchini Tanzania na kote barani Afrika wanachukua nafasi yao stahiki katika kila ngazi ya jamii na kwamba siku za ubaguzi dhidi ya watu wenye ualbino zitakuwa kumbukumbu iliyofifia.

