Sengerema FM
Sengerema FM
14 June 2025, 4:22 pm

Wimbi la wizi wa koki na mita za maji mjini Sengerema limezidi kushika kasi ambapo baadhi ya wezi wamekuwa wakidai kuiba na kuuza kama vyuma chakavu.
Na Emmanuel Twimanye
Mtoto mwenye umri wa miaka 15 katika mtaa wa Busisi Road wilayani Sengerema Mkoani mwanza amekamatwa kwa tuhuma za wizi wa mita na koki za maji.
Akizungumzia tukio hilo mtoto huyo akiwa chini ya ulinzi wa uongozi wa mtaa huo amekiri kuiba mita na koki za maji na kueleza kuwa hiyo ni mara yake ya pili.
Baadhi ya wananchi wamesema kuwa wizi wa mita na koki za maji umekithiri katika mtaa huo na kuiomba serikali kuchukulia hatua kali za kisheria mtoto huyo aliyekamatwa ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia hiyo.
Mwenyekiti wa mtaa wa Busisi Road Agnes Masai amethibitisha kukamatwa kwa mtoto huyo na kumpekeka katika kituo cha Polisi Wilayani Sengerema kwa hatua zaidi za kisheria.