Sengerema FM
Sengerema FM
14 June 2025, 10:19 am

Mai 19 waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Kassimu Majaliwa alikuwa na ziara wilayani Sengerema ya kukagua miradi na kusikiliza kero za wananchi ambapo bodaboda waliiomba serikali kuwasaidia fedha ili kutimiza malengo yao ya kununua koster kwa ajili ya usafirishaji,ambapo waziri mkuu aliahidi kuwachangia mil.10,na mbunge akaahidi mil 10 na jumla ya Tsh. Mil 50 zilipatikana .
Na, Emmanuel Twimanye
Waendesha Pikipiki maarufu Bodaboda katika Jimbo la Sengerema Mkoani Mwanza wamesahauriwa kuangalia namna ya kukata Bima ya afya pamoja na kuchukua mkopo wa Pikipiki ili kuachana na pikipiki za mikataba inayowaumiza .
Ushauri huo umetolewa na mbunge wa Jimbo la Sengerema Mh,Hamis Tabasam katika mkutano wake na wanachama wa umoja wa waendesha Pikipiki uliofanyika katika uwanja wa Tabasam Wilayani Sengerema .
Baadhi ya waendesha Bodaboda wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mh,Hamis Tabasama kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa umoja huo .
Kwa upande wake Kaimu mkuu wa usalama barabarani Wilayani Sengerema Inspekta Norshid Mussa amewaomba waendesha vyombo vya moto kuendelea kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepukana na ajali .
Aidha Mh,Tabasam ametumia mkutano huo kukabidhi shilingi milioni 10 kwa umoja wa waendesha Pikipiki ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za kikundi hicho kwa ajili ya ununuzi wa magari mawili ya umoja huo .