Sengerema FM
Sengerema FM
12 May 2025, 7:57 pm

Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema kinaendelea na oparesheni yake ya No reform No eleections,ambapo tayari imeshaanza kanda ya victoria yenye mikoa ya Kagera,Geita na Mwanza.
Na Emmanuel Twimanye
Makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) bara John Heche amesema chama hicho kitaendelea kushikiria msimamo wake wa kutoshiriki uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu endapo hayatafanyika mabadiliko ya sheria za uchaguzi .
Heche ametoa kauli hiyo leo Mei 12 mwaka huu wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika stendi ya zamani ya mabasi Mjini Sengerema.

Baadhi ya wanachama na viongozi wa chama hicho waliaombatana na makamu mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) bara wameahidi kuendelea kushikiria msimamo huo hadi pale mabadiliko ya sheria za uchaguzi yatakapofanyika.
Aidha Makamu mwenyekiti chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara John Heche anaendelea na ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa kwa ajili ya kuzungumzia kampeni ya chama hicho walioiita No Reforms No election wakimaanisha bila mabadiliko hakuna uchaguzi .
