Sengerema FM
Sengerema FM
30 April 2025, 6:49 pm

Tume huru ya taifa ya uchaguzi (INEC) imetangaza siku saba za wananchi kuboresha taarifa za mpiga kura katika jimbo la Sengerema, mkoani Mwanza.
Na,Elisha Magege
Afsa mwandikishaji jimbo la Sengerema Binuru Mussa Shekidele amewataka maafsa uandikishaji wanaotarajia kwenda kuanza kuboresha taarifa za mpiga kura kuzingatia maadali na kanuni za uandikishaji.
Shekidele ameyasema hayo kwenye semina maalumu kwa ajili ya maafsa uandikishaji iliyofanyika katika ukumbi wa Sengerema Sekondari,ambapo amesema ni vizuri kufanya kazi kwa kuzingatia viapo walivyoapa na kuacha kujihusha na matendo Maovu kwa kipindi cha utekelezaji wa majukumu yao.
Kwa upande wake afsa Mteknolojia msaidizi wa INEC Bi.Eddah Aswile Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao, kwani baada ya zoezi hili hilitarudiwa Tena mpaka uchaguzi mkuu 2030.
Aidha maafsa uandikishaji wamesema wapotayari kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa kwao huku wakiwataka wananchi kujitokeza Kwa wingi kuboresha taarifa zao kwenye daftari la mpiga kura.
Zoezi la uboreshaji wa taarifa za mpiga kura katika halmashauri ya Sengerema linatarajia kuanza tar1/05 na litadumu kwa muda wa siku 7 hivyo kila mmoja anatakiwa kuboresha taarifa zake hasa waliohama maeneo, kupoteza au kuharibu kitambulisho cha awali.
