Sengerema FM
Sengerema FM
20 February 2025, 4:59 pm

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Sengerema (SEUWASA) Imekuwa ikijiendesha kwa hasara kwa muda mrefu jambo lililoibua maswali mengi kwa baadhi ya wananchi mjini hapo, ambapo tayali mamalaka imeanza kuchukua hatua kwa kufuatilia miundo mbinu yake.
Na,Emmanuel Twimanye
Walimu watatu wamekamatwana mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mjini Sengerema (SEUWASA)kwa tuhuma ya wizi wa maji Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.
Meneja utawala na Rasilimali watu wa Mamlaka ya maji Mjini Sengerema Mussa Bujiku amethibitisha kukamatwa kwa walimu hao watatu katika oparesheni iliyoendeshwa na mamlaka hiyo kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Sengerema huku akiwaonya wananachi kuaachana na wizi wa maji ili kuepuka kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Wenyeviti wa serikali za mitaa ,mabalozi pamoja na wananchi wamesikitishwa na kitendo cha baadhi ya watumishi wa serikali kutuhumiwa kujihusisha na wizi wa maji na kuomba vyombo vya dola kuwachukulia hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo.
Baadhi ya walimu waliokamatwa hawakuwa na sababu za msingi za kujieleza .
