Prof. Lyala asherehekea Krismas na wafungwa Magu
26 December 2024, 10:52 am
Wakirsto ulimwenguni kote husherekea sikukuu ya kuzaliwa bwana yesu Kristo kila mwaka tar 25,ambapo pia hufanya matendo mbalimbali ya hisani kwa jamii.
Na,Elisha Magege
Prof.Edwinus Chrisantus Lyaya amekabidhi kitoweo cha Ng’ombe kwa wafungwa katika Gereza la Magu ili washerekee sikukuu ya Christmass 2024.
Akizungumza baada ya kukabizi Ng’ombe huyo kwa mkuu wa magareza ya Magu, Prof.Lyaya amesema msukumo wa kiimani ndio uliomsukuma kutoa kitoweo hicho kwa wafungwa waliopo katika gereza hilo huku akiwasihi watanzania wengine wenye uwezo kukumbuka kusherehekea na ndugu jamaa na marafiki walio kwenye changamoto.
Naye kaimu mkuu wa Magereza Magu SP.Benard Wataye amemshukuru Prof. kwa kuwakumbuka wafungwa, na kuwakumbusha kuhusu suala la utunzaji wa mazingira katika magereza hayo.
Prof. Edwinus Chrisantus Lyaya ni Profesa mshiriki wa Sayansi ya Akiolojia kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam, ambapo pamoja na kutoa kitoweo katika magereza ya Magu pia amepanda miti ya Matunda na kuwahimiza kutunza mazingira katika eneo hilo.