Sengerema FM

Kuelekea miaka 63 ya uhuru Sengerema yafanya usafi hospitali ya wilaya

8 December 2024, 10:14 pm

Viongozi na wananchi wakiendelea na zoezi la kufyeka majani katika eneo la Hospital ya wilaya ya Sengerema.Picha na Elisha Magege

Hivi karibuni waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alielekeza maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania yafanyike Kwa ngazi za Mikoa na Wilaya, kwa kufanya shughuli za kijamii zikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira katika maeneo ya kijamii kama vile hospitali, masoko, kambi za wazee na wenye uhitaji maalumu.

Na;Elisha Magege

Kuelekea miaka 63 ya uhuru wa Tanzania bara, Halmashauri ya Sengerema imefanya usafi katika hospitali ya wilaya Mwabaruhi na kituo cha afya Sengerema.

Akizungumza baada ya zoezi hilo katibu tawala wilaya ya Sengerema Bwn. Cuthibert Midara amesema wilaya ya sengerema mwaka huu inaazimisha miaka 63 ya uhuru kwa kufanya usafi maeneo mbalimbali pamoja na kupanda miti kama kumbukumbu ya maadhimisho hayo.

Sauti ya katibu tawala wilaya ya Sengerema Bwn. Cuthibert Midara akizungumziia maadhimisho ya uhuru 2024

Naye Kaimu mkurugenzi Halmashauri ya Sengerema Wilbert Bandola amewashukuru wananchi na viongozi walio jitokeza leo kufanya usafi katika maeneo ya hospitali licha ya kuwa ni siku ya pumziko.

Sauti ya Kaimu mkurugenzi Halmashauri ya Sengerema Wilbert Bandola akiwashukuruu watumishi wa wananchi walio jitokeza kufanya usafi

Aidha Afsa usafishaji na udhibiti wa taka ngumu mjini Sengerema Bi.Ester Lucas na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali waliojitokeza kufanya usafi siku ya wamewashukuru viongozi wa wilaya kwa kuteua maeneo ya huduma za afya kufanya usafi.

Baadhi ya waananchi na viongozi wakizungumzia zoezi la kufanyya usafi mjini Sengerema