Sengerema FM

Mamlaka ya mji mdogo Sengerema kurejea Chadema wakishinda uenyeviti

26 November 2024, 2:59 pm

Wagombea uenyeviti mjini Sengerema kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Kulia Nuru Lutembeja mgombea mjini kati Sengerema na Bruno Zacharia mgombea Kitongoji Bukala.Picha na Elisha Magege

Kampeni za uchaguzi Serikali za mitaa Mwaka huu 2024 zimeshuhudiwa kuwa na amani bila vurugu yoyote katika halmashauri ya Sengerema huku vyama vyote vikitangaza neema kwa wananchi endapo vitachaguliwa.

Na;Elisha Magege

Mgombea uenyekiti kitongoji mjini kati kupitia Chadema Nuru Lutembeja amewaomba wananchi wa eneo hilo kumchagua ili kuleta maendeleo kwa watu na usafi wa mazingira.

Hayo ameyasema wakati wa mkutano wa kampeni mjini kati eneo la stend ya zamani ambapo amesema kwa mda mrefu eneo la mjini kati limekuwa chafu jambo linaloharibu taswila ya mji wa sengerema.

Sauti ya Nuru Lutembeja mgombea uenyekiti mjini Kati Sengerema

Katika hatua nyingine amesema ataongeza ubunifu wa ajira kwa vijana kupitia Bwawa na kutafuta maeneo yatakayo wawezesha vijana kuwa na sehemu za kujiingizia kipato.

Sauti ya Nuru Lutembeja mgombea uenyekiti mjini Kati Sengerema

Awali akiwaombea kura wagombea, mwenyekiti mstaafu CHADEMA wilaya ya Sengerema Bwn. Buruno Zachalia ambae pia ni mgombea kitongoji cha Bukala, amesema endapo watafanikiwa kuchaguliwa watarudisha mamlaka ya mji mdogo Sengerema.

Sauti ya Bwn.Bruno Zachalia akizungumzia mikakati ya Chama endapo kitapata Lidhaa ya Wananchi

Uchaguzi Serkali za mitaa unatarajia kufanyika nchini jumatano ya Nov 27 ambapo Serikali ya Jamhuli ya Muungano wa Tanzania imetangaza kuwa itakuwa ni siku ya mapumziko kwa watumishi wa umma.