Upepo wa ajabu wavuma na kuangusha kanisa Sengerema
13 November 2024, 8:17 pm
Katika hali isiyo ya kawaida waumini wa kanisa la TEF kwa Neema lililopo katika kitongoji cha Mkomba kijiji cha Busisi, wamejikuta wakiabudia nje baada ya upepo kuvuma ghafla na kudondosha jengo la kanisa lao usiku.
Na;Emmanuel Twimanye
Katika hali isiyokuwa ya kawaida upepo mkali umevuma ghafla na kuangusha kanisa la TFE kwa Neema Mkomba katika kijiji Cha Busisi kata ya Busisi wilayani Sengerema mkoani Mwanza na kusababisha waumini wa kanisa hilo kufanyia ibaada chini ya mti. .
Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya waumini wa kanisa hilo wameshangazwa na kusikitishwa na tukio hilo huku wakiwaomba msaada kwa watu wenye mapenzi mema ili kurejesha kanisa hilo katika hali yake ya kawaida.
Nao baadhi ya viongozi na waumini wa kanisa la AICT Mlimani Mkomba wamelazimika kukatisha ibada na kufika katika kanisa hilo kwa ajili ya kuwafariji huku wakiahidi kuwasaidia ili jengo la kanisa hilo.
Mchungaji wa kanisa la TFE kwa Neema mkomba Timotheo Nziku amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa moja usiku na kusababisha uharibifu wa kanisa hilo na kuwaomba wadau mbalimbali kusaidia vifaa vya ujenzi.
Afisa mtendaji wa Kijiji Cha Busisi Peter Luboya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa pole kwa waumini wa kanisa hilo.
Kufuatia tukio hilo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM ) Wilaya ya Sengerema Mark Agustine Makoye ameahidi kufikia eneo la tukio ili kuona namna ya kutatua changamoto hiyo .