DC Sengerema aongoza wananchi kujiandikisha kushiriki uchaguzi
12 October 2024, 4:23 pm
Serkali kupitia TAMISEMI imetangaza siku kumi za wananchi kujiandikisha kwenye daftari la makazi kwa ajili ya kushiriki uchaguzi serkali za mitaa mwezi november mwaka huu.
Na.Emmanuel Twimanye
Wananachi Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wametakiwa kuendelea kujitokeza kujiandikisha katika Daftari la makazi kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Senyi Nganga wakati akijiandikisha katika daftari la wapiga kura katika kituo cha Shule ya msingi Kilabela na kusema kuwa wananachi hawanabudi kuendelea kujitokeza kujiandikisha ili wapate nafasi ya kushiriki uchaguzi huo.
Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya amewaomba wananachi kutochanganya zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na zoezi lililopita la kuboresha kitambulisho cha mpiga kura kwani kitambulisho hicho kinatumika kwenye uchaguzi mkuu, na kwa wananachi watakaojiandikisha katika daftari la sasa la makazi ndio watakaoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.
Aidha uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu .