Wananchi zaidi ya elf.31 kunufaika na mradi wa Maji chifunfu
11 October 2024, 3:38 pm
Upatikanaji wa maji safi na salama vijijini unasaidia kuimalisha ukuaji wa jamii kiuchumi kwa kupunguza wananchi kutumia muda mwingi kusaka huduma ya maji lakini pia kuchochea maendeleo kupitia kilimo cha umwagiliaji.
Na;Elisha Magege
Wananchi kijiji cha Chifunfu wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wameipongeza serkali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dr.Samia Suluhu Hassani kwa kuwapelekea mradii wa maji safi na salama kutoka ziwa Victoria.
Wakizuungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema wameteseka kwa mda mrefu kwakutumia maji ya ziwani jambo lililopelekea kupoteza ndugu zao kwa kukamatwa na mamba na ndoa zao kuwa matatani kwa kuwaacha waume zao kwenda kutafta maji.
Naye manager wakala wa maji vijijini (RUWASA)Mkoa wa Mwanza Mhandisi Godfrey Sanga amesema mradi wa maji Chifunfu umekamilika kwa asilimia mia moja na kwamba mkoa wa Mwanza unatekeleza miiradi 16 ya maji na itakapo kamilika mkoa utakuwa unatoa maji vijijini kwa asilimia 86.
Aidha Mwenge wa uhuru mwaka huu umefika kwenye mradi huu na kuuzindua huku ukitoa maelekezo ya huduma ya maji kufiikishwa wananchi wote walio karibu na wanaonufaika na mradi huo.
Mradi wa maji kijiji cha Chifunfu ulianza utekelezaji wake mwezi Februari 2022 na umegarimu zaidi ya fedha za kitanzania Tsh.Bilioni 2.9n na utawanufaisha wananchi wapatao elf 31,423 wa vijiji vya Chifunfu,Lukumbi na Nyakahako.