Sengerema FM

UWT Sengerema wapata mwenyekiti mpya

19 September 2024, 1:38 pm

Ester   Petro Maneno  akizungumza na wajumbe wa UWT Sengerema baada ya kumchagua kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo.Picha na Emmanuel Twimanye

Jumuiya ya umoja wa wanawake CCM (UWT) Wilaya ya Sengerema imefanya uchaguzi wa kumpata mwenyekiti mpya kufuatia kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Jane Msoga aliyefariki Dunia April 30, 2024 wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.

Na;Emmanuel Twimanye

Mgombea   wa  kiti  cha  Uenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa wanawake  (UWT)  Wilayani  Sengerema  Mkoani Mwanza    Ester   Petro Maneno  ametangazwa kuwa mshindi wa kiti hicho katika uchaguzi mdogo ili kuziba nafasi hiyo iliyoachwa wazi baada ya mwenyekiti aliyekuwepo  Jane Msoga kufariki Dunia. 

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo  uliofanyika katika ukumbi wa shule ya  Sengerema sekondari  Msimamizi wa uchaguzi  Mwita    Nyarukururu  amemtangaza   Ester Petro Maneno   kuwa  mwenyekiti wa  Jumuiya ya  Umoja wa wanawake Wilaya ya  Sengerema  kwa kupata kura 346, huku mpizani wake Costansia Thomas Faida akipata kura 182.

Msimamizi wa uchaguzi  Mwita    Nyarukururu  akitangaza matokeo ya uchaguzi wa mwenyekiti jumuiya ya wanawake CCM(UWT)Sengerema. Picha na Emmanuel Twimanye
Sauti ya Msimamizi wa uchaguzi  Mwita    Nyarukururu  akitangaza matokeo ya uchaguzi huo.

Ester Petro Maneno  aliyeshinda   uchaguzi huo      amewashukuru wapiga kura kwa kumchagua huku akiahidi  kuwaletea maendeleao.

Sauti ya Mshindi wa kiti cha uenyekiti UWT Sengerema Ndg.Ester Petro Maneno 

Wagombea walioshindwa katika kinyang’anyiro hicho  wamepongeza mchakato wa uchaguzi  huo kwa kufanyika kwa huru na haki.  

Sauti za Wagombea wenza walioshindwa kwnye kinyang’anyilo cha uenyekiti UWT Sengerema.

Aidha  wagombea waliokuwa wakichuana kuwania Kinyanganyiro cha   kiti cha  Uenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa wanawake  Wilaya ya Sengerema  katika uchaguzi huo ni Ester  Petro Maneno  ambaye ameibuka mshindi,Costansia Thomas  Faida ,  Vestina Kanyamtina Chilunga , na Rosemary Matoyo John  wote kutoka chama cha mapinduzi  (CCM) Wilayani Sengerema.

Ester   Petro Maneno  akizungumza na wajumbe wa UWT Sengerema baada ya kumchagua kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo.Picha na Emmanuel Twimanye