Sengerema FM

Matukio ya mauaji ni hatari tuliombee Taifa-Sheikh JAH

13 September 2024, 7:07 am

Sheikh wa wilaya ya Sengerema ambaye pia ni Mwenyekiti kamati ya Amani Ahmad Jah akitoa ushaurii wake juu ya matukio ya utekaji nchini.Picha na Emmanuel Twimanye

Kufuatia kuwepo kwa matukio ya utekaji na mauaji ya raia nchini Tanzania viongozi wa Dini wazidi kuhimiza Waatanzania kila mmoja kwa imani yake kuliombea taifa ili Mungu atuepushe na majanga hayo.

Na;Emmanuell Twimanye

Wananachi  Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wametakiwa kuliombea Taifa  ili kukomesha matukio ya utekaji na mauaji yanayoendelea  kushika kasi katika maeneo mbalimbali hapa nchini .

Kauli hiyo imetolewa na Shekh wa wilaya ya Sengerema ambaye pia ni Mwenyekiti wa  amani Wilayani humo Ahmad Jah   wakati akizungumza na  Radio Sengerema  kufuatia matukio ya utekaji na mauaji  kukithiri na  kuwaomba wananchi kila  mmoja kwa imani yake kuliombea Taifa ili kukomesha matukio hayo.

Sauti ya Sheikh wa wilaya ya Sengerema ambaye pia ni Mwenyekiti kamati ya Amani Ahmad Jah akitoa rai kwa wananchi kumuomba Mungu

Katika hatua nyingine amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuwachukulia  hatua kali za kisheria watu  wanaotekeleza vitendo hivyo.

Sauti ya Sheikh wa wilaya ya Sengerema ambaye pia ni Mwenyekiti kamati ya Amani Ahmad Jah akitoa ushaurii wake juu ya matukio ya utekaji nchini

Naye mwakilishi  wa wenyeviti wa Serikali za mitaa  Wilayani Sengerema  Pelana Bagume  kutoka mtaa wa Geita Road amesema kuwa kwa sasa matukio hayo yamezua taharuki kwa wananachi huku akiwaomba wazazi kuwa makini na watoto wao.

Sauti ya Pelana Bagume Mwenyekiti mtaa wa Geita Road Sengerema

Baadhi ya wananachi wamesema kuwa kwa sasa wanaishi kwa hofu kubwa wakihofia usalama wa watoto wao  na kuiomba serikali kukomesha matukio hayo.

Sauti ya baadhi ya wananchi wilayani Sengerema wakizungumzia hofu yao juu matukio ya utekaji na maauaji