Mwanafunzi adakwa na polisi jamii akiiba simu chuoni Sengerema
10 September 2024, 5:50 pm
Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Sengerema (FDC) ni miongoni mwa vyuo vikongwe nchini vya maendeleo ya wananchi na kimekuwa kikipokea wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Na:Emmanuel Twimanye
Mwanafunzi wa chuo cha Maendeleo ya Wananachi Sengerema (FDC) kilichopo wilayani Sengerema mkoani Mwanza amekamatwa na Polisi Jamii kata ya Nyampulukano kwa tuhuma za kuvamia na kuiba simu za wanachuo wenzake katika chuo hicho .
Akizungumza akiwa chini ya ulinzi wa polisi jamii Paul Samwel mwanafunzi anayetuhumiwa kuiba simu za wenzake amekiri kuiba simu hizo.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho na wananchi wamesikitishwa na tukio hilo na kuiomba jamii kushirikiana kwa pamoja kukomesha matukio hayo.
Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya wananchi (FDC) Wilayani Sengerema Monica Lukeha ameahidi kumfukuza chuo mwanafunzi huyo na kuwaomba wazazi kuendelea kuwafundisha watoto wao maadili mema .
Naye Kamanda mkuu wa Polisi jamii kata ya Nyampulukano Lenatus Lugadija Ngoma amethibitisha Jeshi hilo kumkamata mwanafunzi huyo anayeishi nje ya chuo na kusema kuwa alivamia chuoni hapo majira ya saa tisa usiku wa kuamkia leo na kuiba simu za wanachuo.
Hata hivyo Mwanafunzi huyo amefikishwa katika kituo cha Polisi Wilayani Sengerema kwa hatua zaidi.