Wakatazwa kujihusisha na kilevi wakati wa uandikishaji
20 August 2024, 12:13 pm
Tume huru ya uchaguzi nchini inatarajia kuanza zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la mpiga kura kwa mikoa ya Mwanza na Shinyanga tar21/08/2024
Na:Emmanuel Twimanye
Maafisa uandikishaji wa uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura katika Jimbo la Sengerema Mkoani Mwanza wametakiwa kuzingatia miiko na tarabibu za kazi ikiwemo kutojihusiaha na ulevi sambamba na kutumia lugha zizizokuwa na staha wakati wa uandikishaji ili kuepuka kuharibu zoezi hilo.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa mwandikishaji wa Jimbo la Sengerema Binuru Shekidele wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika ukumbi wa mikutano wa shule ya Sengerema sekondari .
Katika hatua nyingine amewataka kutunza vifaa vitakavyotumika katika zoezi hilo kwa kuwa vimenunuliwa kwa gharamu kubwa.
Awali Afisa uchaguzi wa Tume huru ya uchaguzi Jimbo la Sengerema Yusta Mwambembe amesema kuwa mafunzo hayo yanashirikisha jumla ya washiriki 654 huku akiwapongeza kwa kuchaguliwa katika zoezi hilo.
Nao washiriki wa mafunzo wameahidi kwenda kutekeleza zoezi hilo kwa weledi baada ya kupatiwa mafunzo hayo .
Aidha zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura katika Jimbo la Sengerema linatarajiwa kuanza August 21 hadi 27 mwaka huu likiwa na kauli mbiu isemayo “Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora”