Afariki baada ya kujeruhiwa na kiboko akivua samaki ziwa Victoria
29 July 2024, 7:59 am
Matukio ya watu kujeruhiwa na wanyama wakali wanaoishi majini yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara kwa wakazi wanaoishi kadokando na kufanya kazi ndani ya Ziwa Victoria ambapo wamekuwa wakiiomba Serikali kupitiwa TAWA kuongeza juhudi za kuwawida wanyama hao hasa Kiboko na Mamba.
Na:Elisha Magege
Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina Nyili Katerezi (4O) mkazi kanywengezi kijiji cha Nyandago kata ya Butundwe amefariki Dunia baada ya kujeruhiwa vibaya na mnyama aina ya kiboko wakati akiwa kwenye majukumu ya uvuvi katika mwalo wa Nyandago ndani ya ziwa Victoria.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mwenyekiti wa kitongoji cha kanywengezi Bwn. Enos Makaranga Magoji amesema tukio hilo ni la pili kutokea kwenye kitogoji hicho huku akitoa tahadhali kwa wananchi wanao fanya shughuli zao kandokando ya ziwa kuwa makini na wanyama hao.
Akizungumza kwa niaba ya familia Martini Mlengosha Amesema wamepokea kwa masikitiko tukio la kujeruhiwa kwa ndugu yao na mnyama aina kiboko na kupelekea kupoteza maisha huku wakiiomba serikali kupitia wizara ya maliasili kuweka mikakati thabiti kwa ajili ya kuwazuia wanyama hao ambao kwa maeneo yao ni mara kwa mara wanajitokeza.
Kufuatia tukio hilo mbunge wa Jimbo la Busanda Mhandisi Tumaini Magesa na diwani wa kata hiyo Titos Pamba wamefika kutoa pole kwa familia na kuahidi kulipeka suala hilo kwa waziri mwenye damana husika.
Nao baadhi ya wananchi kijiji hicho wameendelea kuiomba serikali kuliangalia suala hilo kwa umakini mkubwa matukio hayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara.
Aidha katika ajali hiyo iliyotokea majira ya saa kumi usiku chombo walichokuwa wanatumia kuvua walikuwepo watu watatu ambapo wawili walinusirika na mmoja kujeruhiwa vibaya.