Mwenyekiti adaiwa kutafuna fedha za mradi wa kijiji Sengerema
25 July 2024, 11:38 am
Mbunge wa Jimbo la Sengerema Hamis Tabasam amekutana na changamoto hiyo katika ziara yake kata ya Sima, ambapo mwenyekiti wa kijiji hicho anatuhumiwa kutafuna fedha za mradi wa shamba la kijiji.
Na:Emmanuel Twimanye
Mwenyekiti wa kijiji cha Sima wilayani Sengerema Bahati Muhangwa ametuhuhumiwa kutafuna zaidi ya shilingi milioni 5 za mradi wa shamba la mpunga la kijiji hicho lenye ukubwa wa zaidi ya hekari 80.
Tuhuma hizo zimetolewa na baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Kakola B maarufu Ishokela mbele ya Mbunge wa jimbo la Sengerema Mh. Hamis Tabasamu katika mkutano wa hadhara na kusema kuwa mwenyekiti huyo amekuwa akiwakodishia vipande vya mashamba kwa bei ya shilingi laki moja na elfu ishirini kwa kila mmoja huku akidaiwa kutumia fedha hizo kwa matumizi binafsi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Sima Bahati Muhangwa amekanusha madai hayo nakwamba hajatumia fedha kwa matumizi binafsi.
Naye mbunge wa Jimbo la Sengerema Mh,Hamis Tabasam ameahidi kupeleka mkaguzi wa ndani kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa fedha hizo.