Wananchi watakiwa kuanzisha miradi ya maendeleo
17 July 2024, 4:12 pm
Zaidi ya Bilioni.929 zimeletwa na Serkali ya awamu ya sita kutekeleza miradi ya maendeleo wilayani Sengerema,ikiwemo miradi ya kukamisha na mipya.
Na;Elisha Magege
Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Sengerema mkoani Mwanza Binuru Mussa Shekidele amewataka wananchi kubuni na kuanzisha miradi ya maendeleo ili Serkali iikamilishe miradi hiyo.
Mkurugenzi ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya misheni mjini Sengerema ambapo amesema serikali imepeleka fedha nyingi maeneo mbalimbali ya halmashauri kwenda kukamilisha miradi iliyoanzishwa na wananchi hivyo ni vyema sasa wananchi wakaanzisha miradi itayosaidia halmashauri kuomba fedha kwa ajili ya miradi hiyo.
Katika hatua nyingine Shekidele amewataka wazazi na walezi kufuatilia mienendo ya watoto wao dhiidi ya mumomonyoko wa maadili ambao umekua ukitokea kwa vijana nchini.
Kata ya misheni ni miongoni mwa kata 25 zinazounda halmshauri ya Sengerema na imepata fedha za mradi wa ujenzi shule mpya ya matwiga iliyopo eneo la Mwabayanda.